Wataalamu wengi wamezungumza kuhusiana na suala la madhara ya kahawa mwilini. Hayo yakiendelea Jaji mmoja nchini Marekani ameeleza kuwa kahawa inatakiwa itengenezewe tahadhari ya saratani.
Jaji huyo ameeleza kuwa japokuwa ushahidi wa kwamba kahawa ina madhara au lah bado haujawa wazi, watengenezaji wa kahawa wanatakiwa kuweka vikaratasi vya tahadhari kwenye bidhaa hiyo.
Sheria ya Maji Safi nchini humo inaeleza kuwa inahitaji kuwekwa lebo za tahadhari kwenye vinywaji vyote vyenye kemikali aina takribani 900 zinazojulikana kwa kusababisha saratani na matatizo ya uzazi.
0 Maoni